Kumbuka: Kuendelea kutumia mfumo huu kunamaanisha umesoma na kukubali vigezo hivi. Kutokuyasoma kwa umakini hakutakuwa sababu ya kudai hukuyajua.
01. Terms & Conditions
Huduma & MatumiziKaribu VIONEX TRADERS COMPANY LTD. Tunatoa jukwaa la biashara na huduma zinazolenga kurahisisha malipo, uagizaji na usafirishaji wa bidhaa/huduma kwa ufanisi. Masharti haya yanalinda haki zako na kuweka misingi ya uaminifu kati ya kampuni, vendors na wateja.
Payments & Transactions
Malipo yafanyike kupitia njia rasmi zilizoidhinishwa.
Malipo yote ya bidhaa na huduma lazima yafanyike kupitia mifumo rasmi iliyo ndani ya tovuti au njia tulizoidhinisha. Kampuni haitawajibika kwa malipo yaliyofanywa nje ya mfumo rasmi au kupitia maelekezo yasiyo sahihi.
Delivery & Logistics
Usafirishaji huanza baada ya malipo kuthibitishwa.
Baada ya malipo kuthibitishwa kikamilifu, mzigo utaandaliwa na kusafirishwa kulingana na anwani iliyotolewa na mteja. Muda wa delivery unaweza kutofautiana kulingana na eneo, hali ya usafiri na taratibu za usafirishaji.
Product Usage
Matumizi ya bidhaa yafanyike kwa kufuata maelekezo.
Mteja anawajibika kutumia bidhaa kwa madhumuni halali na kwa kufuata maelekezo ya matumizi. VIONEX TRADERS COMPANY LTD haitahusika na madhara yatokanayo na matumizi yasiyo sahihi au kinyume na maelekezo.
Liability & Responsibility
Uwajibikaji hutegemea sheria na uthibitisho.
Kampuni haitawajibika kwa hasara za moja kwa moja au zisizo za moja kwa moja zitokanazo na matumizi ya bidhaa baada ya kuwasilishwa, isipokuwa pale ambapo sheria itahitaji vinginevyo.
Security & Compliance
Linda OTP na nywila zako muda wote.
Tunatumia teknolojia za kisasa kuhakikisha usalama wa taarifa zako binafsi na miamala yako. Mtumiaji anatakiwa kulinda taarifa zake za siri ikiwemo OTP na nywila; usizitoe kwa mtu mwingine.
Masasisho ya Masharti
Tunaweza kusasisha sera kwa maslahi mapana.
VIONEX TRADERS COMPANY LTD ina haki ya kurekebisha au kusasisha masharti haya wakati wowote. Mabadiliko yatatangazwa kupitia tovuti yetu na yataanza kutumika mara moja baada ya kuchapishwa.
Ushauri: Tumia njia rasmi za malipo pekee, hakiki anwani kabla ya ku-confirm order, na wasiliana na support mapema ukikumbana na changamoto.
02. Privacy Policy
Faragha & DataVIONEX TRADERS COMPANY LTD inaheshimu na kulinda faragha ya wateja wake. Sera hii inaeleza jinsi tunavyokusanya, kutumia, kuhifadhi na kulinda taarifa zako binafsi unapofanya matumizi ya tovuti na huduma zetu.
๐งพ Taarifa tunazokusanya
Tunakusanya taarifa muhimu pekee zinazohitajika ili kukuwezesha kupata huduma zetu kwa usahihi, usalama na ufanisi.
- ๐ค Jina kamili la mtumiaji
- โ๏ธ Barua pepe (Email)
- ๐ฑ Namba ya simu ya mawasiliano
- ๐ Anwani ya delivery (kwa uwasilishaji wa bidhaa)
๐ฏ Matumizi ya taarifa
- Kuthibitisha miamala na usalama wa akaunti.
- Kuratibu na kuwasilisha bidhaa/huduma ulizoomba.
- Kutoa huduma kwa wateja na kuboresha uzoefu wa mfumo.
๐ Usalama wa taarifa
Tunatumia hatua za kiusalama (ikiwa ni pamoja na udhibiti wa ufikiaji na ufuatiliaji wa miamala) kulinda taarifa dhidi ya upotevu, matumizi mabaya au ufikiaji usioidhinishwa. Mtumiaji anahimizwa kulinda nywila na OTP zake.
๐ค Ushirikishwaji wa taarifa
Hatushughuli kutoa wala kushiriki taarifa zako binafsi kwa mtu au taasisi nyingine bila idhini yako, isipokuwa pale inapohitajika kisheria au kwa utekelezaji wa huduma uliyoomba (mfano: usafirishaji/udhibitisho wa miamala).
Marekebisho ya sera: Sera hii inaweza kurekebishwa mara kwa mara; mabadiliko yatatangazwa na kuanza kutumika mara moja baada ya kuchapishwa.
03. Billing Policy
Malipo & RisitiSera hii inaeleza kwa uwazi namna VIONEX TRADERS LTD inavyoshughulikia malipo, ada za delivery na marejesho ya fedha. Lengo letu ni kukupa uzoefu wa malipo ulio salama, rahisi na unaoaminika.
Payment Methods
Njia salama na rasmi pekee.
Malipo yanapokelewa kupitia njia salama na rasmi ikiwemo USSD, Mobile Money na mifumo mingine iliyoidhinishwa. Hatukubali malipo ya moja kwa moja kwa mtu binafsi ili kuhakikisha usalama wa fedha zako.
Delivery Fee
Ada ya delivery (kama ilivyoainishwa).
Ada ya delivery ni 10% ya thamani ya bidhaa uliyoagiza. Ada hii inahusisha gharama za maandalizi, usafirishaji na ufuatiliaji wa mzigo wako hadi ufikishwe salama kwenye anwani uliyochagua.
Refund Policy
Marejesho hufuata tathmini na uthibitisho.
Marejesho ya fedha (refund) yatafanyika endapo bidhaa itabainika kuwa na tatizo lililothibitishwa au kinyume na maelezo ya awali. Kila ombi la refund hupitiwa kwa umakini ili kuhakikisha haki na uwazi kwa pande zote.
Billing Transparency
Risiti halali yenye QR (kama mfumo unavyoruhusu).
Tunahakikisha muamala una risiti halali yenye QR Code kwa uthibitisho (kulingana na utekelezaji wa mfumo). Hii hukupa kumbukumbu salama za manunuzi yako.
Ahadi Yetu: Uwazi, usalama na uaminifu. Tumia mifumo rasmi pekee, na wasiliana nasi mara moja endapo kutatokea changamoto yoyote ya malipo au billing.
Vendor anatakiwa kutumia jukwaa la VIONEX TRADERS COMPANY LTD kufanya biashara halali kwa mujibu wa sheria na taratibu za kampuni. Vendor anapaswa kutoa huduma stahiki kwa wateja wote bila ubaguzi wowote (kabila, urafiki, au vigezo visivyo halali).
- Vendor ahakikishe mawasiliano na mteja yanafanyika kwa uadilifu, heshima na faragha.
- Vendor ahifadhi taarifa za wateja kwa usiri; asizitumie vibaya wala kuzisambaza kinyume na sera.
- Vendor amfahamishe mteja kwamba kuna uwezekano kampuni au mamlaka kutumia taarifa za mteja pale inapohitajika kisheria.
Uthibitisho wa vendor: Vendors wanaweza kuhitajika kuwasilisha nyaraka rasmi (mf. NIDA, leseni, cheti cha biashara, barua ya utambulisho, n.k.) kwa lengo la kuthibitisha uhalali wa biashara na kuimarisha uaminifu wa mfumo.
05. Kufubaza (Freeze) na Kufuta (Suspend) Akaunti ya Vendor
Ulinzi wa MfumoVIONEX TRADERS LTD ina haki ya kuchukua hatua za kiusalama kulinda jukwaa, wateja na vendors. Akaunti ya vendor inaweza kufubazwa kwa muda au kusimamishwa (au kufutwa) endapo kutabainika ukiukwaji wa vigezo.
- Vendor akitumia jukwaa kufanya biashara isiyosajiliwa au kinyume na aina ya biashara aliyosajili wakati wa kujiunga na VIONEX TRADERS.
- Vendor akishindwa kumhudumia mteja au kushughulikia tatizo halali la mteja bila sababu za msingi, na mteja akatoa taarifa (report) kwa HQ kwa ushahidi unaoaminika kutoka pande zote.
Utaratibu wa tathmini: Akaunti inaweza kufubazwa kwa muda wa uchunguzi usiopungua siku 3 na usiozidi siku 15. Bodi/Usimamizi unaweza kuitisha kikao cha dharura kupitia njia rasmi (mf. Google Meet/Zoom) kwa ajili ya kufanya uamuzi wa mwisho kulingana na ushahidi na taratibu za kampuni.
04A. Huduma za Ziada kwa Vendors
Vendor ToolsKwa vendors wa VIONEX TRADERS COMPANY LTD, tumetengeneza huduma za ziada zinazosaidia kurahisisha mawasiliano na kuongeza uaminifu kati ya vendor na mteja. Huduma hizi zinapatikana kwa upande wa vendors na wateja wao tu, na zinalenga shughuli halali za kibiashara ndani ya mfumo.
Video Call (Live)
Mawasiliano ya moja kwa moja ndani ya VIONEX.
Vendor anaweza kupiga video call live ndani ya VIONEX ili kuongea na mteja kwa urahisi. Huduma hii hutumika pale tu ambapo kuna shughuli halali za biashara zinaendelea, na inapatikana kwa vendor ambaye tayari amethibitishwa (verified) na HQ ya VIONEX TRADERS COMPANY LTD.
Live Chat
Chat ya papo kwa papo bila usumbufu.
Vendor na mteja wake wanaweza kuchati kwa live ndani ya mfumo wa VIONEX endapo wote wanatumia mfumo. Hii husaidia kurahisisha maswali, majibu na ufuatiliaji wa oda.
Google Location Link
Wateja kukufikia kwa urahisi.
Vendor anaweza kuweka Google Maps location link ili mteja apate njia ya kukufikia kwa urahisi pale inapohitajika kwa makubaliano ya biashara na delivery.
Blue Verified Badge
Kuongeza uaminifu kwa wateja.
Vendor akiwa active member na amekamilisha uthibitisho, atapata Blue Verified Badge kwa lengo la kuimarisha uaminifu na ubora wa huduma zake.